BMT YATOA MAELEKEZO KWA VIONGOZI WA TACA
service image
24 Mar, 2024

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limewapa maelekezo viongozi wapya wa Chama cha Makocha wa Riadha Tanzania (TACA) kurekebisha katiba yao kwa maendeleo ya michezo nchini.

Maelekezo hayo yametolewa leo Machi 24, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa BMT Charles Maguzu, baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliofanyika jijini Dodoma.

Àidha, Maguzu amewasisitiza Viongozi hao kushirikiana kwa maslahi ya Chama, lakini pia kushirikiana na Serikali katika masuala mbalimbali ili kufikia malengo ya chama hicho.

"Kingine tuombe mkaongoze kwa uwazi kwa kila jambo ili chama kiweze kusonga mbele,"

Aliendelea kwa kuwataka viongozi hao kujiendeleza kwa kupata mafunzo pamoja na kuhakikisha wanariadha wao wanaingie nao mikataba wanapo wafundisha ili kuepusha migogoro ya baadaye.

Viongozi hao watakaodumu kwa muda wa miaka minne madarakani wametakiwa pia kutekeleza majukumu ya chama kwa mujibu wa katiba yao pamoja na kuwa wabunifu wa kutafuta vyanzo vya fedha za kukiendesha chama kwa maendeleo zaidi