BMT, JICA NA TIKA WAIMARISHA NA KUKUZA MCHEZO WA GOALBALL MASHULENI
service image
10 Mar, 2026

 

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japani (JICA) pamoja na Shirika la Ushirikiano na Uratibu la Uturuki (TIKA), leo tarehe 10 Machi 2026 wametembelea shule 9 kati ya shule 15 zilizopatiwa mafunzo ya mchezo wa GoalBall kwa walimu wa michezo wa shule za msingi na sekondari mkoani Dar es Salaam.

 

Katika ilikagua na kufatilia namna mafunzo hayo yanavyotekelezwa mashuleni pamoja na kukabidhi mpira wa GoalBall kwa kila shule ili kusaidia kuendeleza mchezo huo kwa vitendo.

 

Shule zilizotembelewa ni pamoja na Shule ya Sekondari Pugu, Shule ya Sekondari Kitonga, Shule ya Msingi Pugu Kajiungeni, Shule ya Msingi Maarifa, Shule ya Msingi Airwing, Shule ya Msingi Mzambarauni, Shule ya Msingi Viwege, Shule ya Msingi Zingiziwa na Shule ya Msingi Yange Yange.

 

Ziara hiyo imelenga kufuatilia utekelezaji wa mafunzo yaliyotolewa kwa walimu wa michezo kuhusu mchezo wa GoalBall, sambamba na kuhamasisha maendeleo na usambazaji wa mchezo

huo katika shule mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam.

 

Jitihada hizi ni sehemu ya ushirikiano wa kimataifa unaolenga kuimarisha sekta ya michezo nchini pamoja na kuwapa vijana fursa ya kushiriki na kukuza vipaji vyao kupitia michezo.