BMT NA BASATA WAKUTANA NA CCST KUJADILI FURSA ZA AFCON 2027
06 May, 2026
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msitha, pamoja na Kaimu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Edward Buganga, wamekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Chama cha Salonist Tanzania (CCST), leo Mei 6, 2026 jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, pande zote zimejadili masuala mbalimbali ya chama hicho, ikiwemo uzinduzi wake pamoja na mikakati ya kutumia fursa zitakazotokana na AFCON 2027.
Aidha, kikao hicho kilihudhuriwa pia na mdau wa masuala ya urembo na utanashati, Jokate Mwegelo, ambaye ni balozi wa chama hicho, akisisitiza umuhimu wa sekta ya urembo kuchangamkia fursa za kimataifa kupitia michezo.

