BMT YAPOKEA CHETI CHA SHUKRANI KUTOKA TLGU
service image
21 Dec, 2023

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Benson Chacha, leo tarehe 21 Disemba, 2023 amepokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa rais wa Chama cha Gofu Wanawake (TLGU) Queen Siraki, kwa mchango mkubwa ambao Serikali imekuwa ikitoa kwa Chama hicho cha mchezo wa Gofu wanawake Tanzania.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za BMT zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.