BMT YAKUTA NA WADAU WA MBIO ZA KILI MARATHON 2026 KUFANYA TATHIMINI
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeendesha kikao maalum kujadili mafanikio na changamoto za mbio za Kili Marathon 2026, zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.
Kikao hicho kimefanyika Mei 5, 2026 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na kuongozwa na Afisa Michezo Mwandamizi wa BMT, Bw. Charles Maguzu.
Wadau mbalimbali walishiriki katika kikao hicho, wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Jeshi la Polisi, Shirikisho la Riadha Tanzania, pamoja na viongozi wa Halmashauri za Moshi Municipal na Moshi District, na waandaaji wa mbio hizo.
Majadiliano yalilenga kuboresha maandalizi ya mbio zijazo, kuimarisha usalama, na kuongeza ubora wa tukio hilo ambalo linaendelea kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mchezo wa riadha.

