BMT YAKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA MISHALE
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limekutana na Uongozi wa Chama cha Mchezo wa Mishale katika kikao kilichofanyika Mei 5, 2026, jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulihudhuriwa na maafisa wa BMT kutoka kitengo cha usajili wa Vyama vya Michezo, pamoja na viongozi wa chama hicho wakiongozwa na Rais wa Bw. Kelvin Fredinand Tresphory.
Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Shirikisho la Mchezo wa Kurusha Mishale zilizopo Morocco, jijini Dar es Salaam, kikilenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo usajili, maendeleo na uimarishaji wa mchezo huo nchini.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, upande wa BMT Bi. Hellen Kaaya Afisa Michezo alisisitiza umuhimu wa vyama vya michezo kuzingatia taratibu na kanuni zilizowekwa ili kuhakikisha vinafanya kazi kwa ufanisi.
Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Baraza la Michezo la Taifa katika kusimamia na kuendeleza sekta ya michezo nchini, ikiwa ni pamoja na kukuza na kuimarisha michezo mbalimbali kwa manufaa ya taifa.

