CAF WAKAGUA MIUNDOMBINU ITAKAYOTUMIKA AFCON 2027
Timu ya wataalamu kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Jana Julai 30 ,2023 imefanya ukaguzi wa miundombinu ya michezo ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027.
Akifungua kikao cha kuwakaribisha wataalam hao, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali ya Tanzania ipo tayari kuandaa michuano hiyo pamoja na Kenya na Uganda kwa kuwa uamuzi huo umefanyiwa kazi katika ngazi ya juu ya serikali.
“Mimi binafsi niliwasilisha ajenda hii katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri wote na ilipitishwa kwa kauli moja na maagizo yakatolewa kwamba tuendelee na taratibu za kuandaa mashindano haya” amesema Balozi Dkt. Chana.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Saidi Yakubu amesema tayari Serikali imesaini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao utagharimu Sh. Bilioni 31, ili kufanikisha azma hiyo ambayo ni sehemu ya Umoja wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki .
Ukaguzi umefanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Julius Nyerere, hospitali ya Taifa Muhimbili, Uwanja wa Uhuru, na viwanja vingine vya