CHANGALAWE ASHINDA MEDALI YA FEDHA NA DOLA $3,000 KATIKA MASHINDANO YA MANDELA CUP.
service image
22 Apr, 2024


Nahodha wa kikosi cha 'Faru Weusi wa Ngorongoro' Yusuf Changalawe amefanikiwa kushinda medali ya fedha licha ya kupoteza pambano lake la fainali dhidi ya Pita Kabeji wa kutokea DR Congo kwa matokeo ya 'split decision ya bout review' (Matokea ya kurudiwa) ya points 4-3 katika mashindano ya Mandela Cup ndani ya Jiji la Durban, Afrika ya Kusini.

Pambano hilo la uzani wa Light Heavyweight 80kg ni la pili kuwakutanisha Changalawe na Kabeji huku Changalawe akipoteza kwa mara ya pili dhidi ya Kabeji baada ya pambano la awali la nusu fainali katika mashindano ya Afrika Accra 2023 lililofanyika mwezi uliopita.

Changalawe amefanikiwa kupata medali ya Fedha na zawadi ya pesa Dola $3,000 (Tzs 7,800,000)

Wakati huohuo Bondia Azizi Waziri Chala aliyeshika nafasi ya tatu baada ya kupoteza pambano lake la nusu fainali dhidi ya Trofimus Johannes kwa points 5-0 amefanikiwa kupata medali ya Shaba na zawadi wa pesa ya Dola $1,500 (3,800,000)

Tanzania iliwakilishwa na wachezaji 5 ambao ni Ezra Mwanjwango, Musa Maregesi, Yusuf Changalawe, Aziz
Mashindano hayo ya Mandela yamefikia tamati usiku wa Aprili 21, 2024 na Timu inatarajiwa kusafiri tarehe 22 Aprili kutoka Durban kurejea Dar es salaam kwa Shirika la Ndege la Airlink kupitia Johannesburg na inatarajiwa kufika majira ya saa 8.30 usiku.