CHANGALAWE AMCHAKAZA MVENEZUELA

05 Mar, 2024
Bondia Yusuf Changalawe ameanza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kushinda pambano lake la kwanza dhidi ya Pereira Diego kutoka Venezuela kwa *KO* round ya kwanza, dakika ya 01 na kufanikiwa kutinga kibabe hatua ya 32 bora katika uzani wake wa Light Heavyweight 80kg katika mashindano ya kwanza ya Dunia ya kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024 yanayoendelea nchini Italia.