CHANGALAWE ASHINDA NA KUTINGA ROBO FAINALI KUFUZU PARIS OLIMPIKI 2024
service image
10 Sep, 2023

Kapteni wa Timu ya Taifa ya Ngumi na mshindi wa medali ya Shaba Ubingwa wa Afrika 2023 Yusuf Changalawe ameshinda kwa points 5-0 dhidi ya mpinzani wake Mpi Anauel Ngamissengue kutoka Congo Brazzaville katika uzani wa 80Kg.

Sasa Changalawe ameingia hatua ya robo fainali ya mashindano ya kufuzu Paris Olimpiki 2024 yanayoendelea katika Jiji la Dakar, Senegal ambapo jumla ya nafasi za awali 18 za kufuzu kushiriki Olimpiki kwa Bara la Afrika zinagombewa.