KAMATI YA KUWEKA MIPANGO YA KUANDA TIMU KUELEKEA AFCON 2027
08 Nov, 2024
Kamati maalumu ya kupanga mipango ya kuandaa timu ya mpira wa miguu ya U17, U20 na U23 kuelekea AFCON 2027 pamoja mashindano mengine ya Dunia ambayo timu za Tanzania zitakwenda kushindana, leo Nov 08, imeahirisha kikao hicho kwa kuweka bajeti itayowasilishwa mapema kwa Wizara na taasisi husika kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu lengwa.
Aidha, sanjari na kuahirisha kikao hicho Wajumbe wamezishauri TAMISEMI na TFF kuimarisha mahusiano na kuwa wazi katika ratiba zao za mashindano ili zipishane kwa lengo kutafuta vipaji kwa pamoja ili kuifanya nchi kufanikiwa katika AFCON 2027 pamoja na mashindano mengine kimataifa.