HONGERA SANA KWA KUIPEPERUSHA BENDERA YA NCHI KWA USHINDI
service image
14 Nov, 2023

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Judo Andrew Thomas Mlugu anaecheza uzito wa 73 Kg amefanikiwa kushinda medali ya Fedha baada ya kumaliza mshindi wa pili katika mashindano ya wazi ya Afrika (African Open Championship) yanayoendelea Dakar nchini Senegal.

Ushindi huo umeiwezesha Tanzania kupanda kiwango (rank) hadi nafasi ya 12 Barani Afrika.