DKT. NDUMBARO ASISITIZA WADAU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUENDELEZA MICHEZO NCHINI
service image
20 Sep, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo tarehe 20 Septemba, 2023 amekutana na viongozi wa timu ya Simba ambapo wamejadili masuala mbalimbali yakiwemo maendeleo ya michezo nchini.

Kikao hicho pia kimejadili maandalizi ya michuano ya Africa Football League ambayo timu ya Simba inashiriki ikiwa miongoni mwa timu nane bora Afrika.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Ally Mayay, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Yotham Msitha, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw. Wilfred Kidau, Mtendaji Mkuu wa Timu ya Simba Bw. Imani Kajula pamoja na viongozi wengine