DROGBA AAGA TANZANIA, AACHA ALAMA YA KIMATAIFA
06 May, 2026
Nyota wa zamani wa soka, @didierdrogba , aliyewahi kung’ara katika klabu ya Chelsea F.C. na timu ya taifa ya Ivory Coast, ameondoka nchini Mei 5, 2026.
Drogba alikuwa nchini kufuatia mwaliko wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, ambapo alipata fursa ya kuhudhuria uwasilishwaji wa Hotuba ya Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Ziara ya nyota huyo imeacha alama kubwa, ikiendelea kuimarisha taswira ya Tanzania katika anga la michezo kimataifa, hususan katika kuelekea mashindano ya AFCON 2027.

