HAFLA YA KUIPONGEZA TAIFA STARS
service image
10 Jan, 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanaume ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Rais Mhe. Dkt. Samia aliwaandalia hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri kimataifa, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 10 Januari 2026.

Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ilishiriki kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ nchini Morocco na kufika hatua ya mtoano, ambayo ni historia kubwa kwa Tanzania tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo.