HAFLA ZA KUTUNUKIWA MEDALI KUFANYIKA LEO.

Hafla za kutunukiwa medali kwenye mchezo wa ngumi katika kila uzani zitafanyika siku ya leo wakati wa mapambano ya fainali.
Tanzania 🇹🇿 itapata rasmi *medali mbili (2)* leo kupitia Mabondia wake wawili *Kassim Mbundwike* aka "Mfupa wa Sokwe" na *Yusuf Changalawe.*
Hafla ya kwanza kwa Tanzania itakua majira ya Uingereza saa 6:45 mchana *(Tanzania 8:45 mchana)* katika uzani wa Light heavyweight 75kg - 80kg ambapo *CHANGALAWE* atatunukiwa medali ya *SHABA* 🥉 (Bronze)
Hafla ya pili kwa Tanzania itafanyika majira ya Uingereza saa 10:30 jioni *(Tanzania saa 12:30 jioni)* katika uzani wa Light middleweight 67kg - 71kg ambapo Bondia *MBUNDWIKE* atatunukiwa medali ya *SHABA* 🥉(Bronze)
Mpaka kufikia sasa nchi ya *TANZANIA* imefanikiwa kushinda medali tatu (3), ambapo mbili (2) za Shaba 🥉 zimetokana na mchezo wa Ngumi na medali moja (1) ya fedha 🥈 ambayo imetokana na mchezo wa riadha kupitia kwa *Felix Simbu.*
Mara ya mwisho nchi yetu kupata medali katika michezo hii ya Jumuiya ya madola ilikua ni *miaka 16* iliyopita katika michezo ya *Melbourne 2006 (Dhahabu 1 na Shaba 1)* na kurudi mikono mitupu New Delhi 2010, Glasgow 2014 na Gold Coast 2018.