Hakika ni Heshima kubwa sana kwa Mheshimiwa Rais
service image
05 Jun, 2022

TIMU ya Taifa ya wasichana chini ya umri wa miak 17, Serengeti Girls imefanikiwa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Cameroon Jumapili Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katika mchezo huo wa marudiano Raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya Fainali zitakazofanyika Oktoba  2022 nchini India, bao pekee la Tanzania lilifungwa na Neema Paul Kinega.
Serengeti Girls inafuzu Fainali za kwanza za Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla wa 5-1 kufuatia kushinda 4-1 kwenye mechi ya kwanza Yaoundé.

Kufuzu huko kumemheshimisha Rais Samia ambaye katika utawala wake amewekeza sana katika michezo ikiwemo ya wanawake.