MHE.DR. NDUMBARO AIAGIZA BMT KUONGEZA MICHEZO MINGINE KATIKA MICHUANO YA 'LADIES FIRST'.
service image
25 Nov, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro ametoa maagizo kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kuhakikisha wanaongeza michezo mingine katika mashindano ya 'Ladies First'.

Kauli hiyo ametoa Novemba 25, 2023 wakati anafungua mashindano ya riadha ya wanawake msimu wa tano 'Ladies First' yaliyoanza tarehe 24 hadi 26 Novemba, 2023 jijini Dar es Salaam.

Amesema Shirika la Maendeleo ya Ushirikiano wa Kimataifa la Japan 'JICA' ndiyo wanadhamini mchezo wa riadha upande wa Tanzania jukumu lao ni kuongeza michezo mingine.

"Tuongeze mchezo wa soka, ngoma na muziki, rede, mdako kwa wanawake ikiwezekana tunatakiwa viongozi wanawake wanasiasa siasa wawepo kwa sababu hili jambo la wanawake, "alisema.

Aidha, Dk. Ndumbaro ametoa wito kwa vyama vya michezo kuhakikisha wanaendeleza michezo ikiwemo kutafuta vyanzo vya fedha ambazo vitasaidia timu za taifa kushiriki vyema mashindano ya kimataifa.

Alisema BMT na Serikali ni waratibu wa michezo lakini ndiyo watu wa kwanza kuhakikisha wanatafuta mapato ya fedha kwa lengo la kuendeleza michezo hiyo.

"Pongezi Kwa Chama Cha riadha 'RT' Kwa kutafuta wadhamini wa mashindano haya kwa kushirikiana na Japan,"alisema.

"Pia pongezi kwa mwanariadha mkongwe, Juma Ikangaa kwa kuleta Wazo hili la kuendeleza vipaji vya wanawake nchini, kuanzia leo mashindano haya yatakuwa yanaitwa 'Juma Ikangaa Ladies First 'kutokana na mchango wake mkubwa na kuwaleta JICA kuwa wadhamini, "alisema.

Waziri Ndumbaro aliongeza kwa kusema kuwa, michezo inaongeza uchumi na kuleta ajira kwa vijana pamoja na kulinda mwili kutokana na mazoezi unayofanya.