MAFUNZO YA KABADDI ZANZIBAR
service image
09 Feb, 2024

Mafunzo ya mchezo wa Kabaddi yanayoratibiwa na chama cha mchezo wa Kabaddi Tanzania kwa ushirikiano na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) yameendelea kuchanja mbuga ambapo kwa sasa yanaendeshwa Zanzibar.

Mafunzo hayo yameanza tarehe 8 Februari na yatahitimishwa 14 Februari, 2024 yakihusisha washiriki 70 wakiwemo walimu wa michezo wa shule za sekondari na msingi pamoja na washiriki kutoka katika majeshi yaani JKU, KMKM, KZU, Zimamoto na JWTZ sanjari na wachezaji wa awali ambao ni raia.