KIKAO CHA BODI

28 Oct, 2022
Mwenyekiti wa bodi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Leodegar Chila Tenga leo tarehe 28 Oktoba, 2022 amekutana na wajumbe wa bodi ya BMT pamoja na sekretarieti kupitia miongozo, maelekezo na taarifa mbalimbali zenye lengo la kuweka mikakati bora ya kuendelea kupiga hatua katika michezo nchini.
Aidha, kikao hicho kilihudhuriwa na Makamu Mwenyekiti Prof. Mkumbukwa Mtambo, Neema Msitha Katibu na wajumbe Ally Mayay, Tuma Dandi, Ameir Mohammed pamoja na sekretarieti ya Baraza ambao ndio watekelezaji wa maelekezo yote.