KIKAO CHA KUENDELEZA USHIRIKIANO
service image
24 Aug, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha Agosti 23, 2023 kwa niaba ya Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo amefanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Serikali ya China kupitia wawakilishi wake waliopo katika Ubalozi wa nchi hiyo nchini Tanzania kuhusu kuendeleza ushirikiano katika sekta tofauti nchini.

Aidha, katika mazungumzo yao wamekusudia kuandaa tukio kubwa mwaka 2024 litakalohusisha sekta ya Utamaduni na Utalii baada ya kuingia makubaliano kati ya serikali hizo.