KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTAMADUNI NA MICHEZO

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha akijibu maswali ya wadau wa kikao kazi cha 13 cha Maafisa Utamaduni na Michezo kinachoendelea kwa siku 3 kuanzia leo Aprili 04 hadi 06 Jijini Dodoma.
Maswali yaliyoulizwa na Maafisa hao baada ya Afisa Michezo wa BMT Apansia Lema kuwasilisha mada yake kuhusu mabadiliko ya kanuni cha usajili ambapo maswali yaliulizwa kuhusu kutofanyika kwa mikutano ya kamati za michezo za mikoa, pamoja usajili kuchelewa.
Katika hayo Katibu Mtendaji wa BMT Neema Msitha ameeleza kuwa vikao vya kamati za mikoa vimekuwa vikifanyika na baada ya kikao kazi hiki kikao hicho kitafanyika ambacho huwa kinahusisha wenyeviti wa Michezo wa Mikoa (MARAS).
Lakini pia kuhusu suala la usajili kucheleweshwa, Msitha amemshukuru Mhe. Waziri mwenye dhamana ya michezo kumtangaza msajili tarehe 29 Machi, 2022 ambaye kwa muda mrefu hakuwepo na ndiyo sababu ya kucheleweshwa, na kusema kuwa changamoto ya usajili kwa sasa itakuwa imetatuliwa.