KIKAO KUELEKEA KATIKA SIKU MUHIMU KWA MAVETERANI WA SOKA NCHINI.
service image
12 Apr, 2024

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa kushirikiana na Umoja wa Maveterani Tanzania (UMSOTA) tarehe 12 Aprili, 2024 wamekaa kikao cha maandalizi kuelekea katika siku muhimu kwa wanasoka hao wa zamani, tukio la kupewa Bima za Afya kutoka kwa Shirika la Bima la Taifa ( NHIF) litakalofanyika Aprili 25, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimewahusisha Afisa Michezo wa BMT Charles Maguzu akimwakilisha Katibu Mtendaji pamoja na wanasoka wa zamani na Viongozi wa UMSOTA akiwemo, Mwenyekiti Paul Ambrose Lusonza, Mweka hazina Alhaj Eng.Abdullah Fereshi Abdullah, Salum Mwinyimkuu aka (Carlos) na Rahim Lumelezi (Wajumbe).