KING LUCAS MWAJOBAGA ALIHESHIMISHA TAIFA NCHINI TUNISIA KWA USHINDI WA MKANDA
service image
25 Jan, 2025

Bondia Lucas Mwajobaga amefanikiwa kuibuka na ushindi wa kibabe dhidi ya Liduema Elder kutoka Angola katika mapambano ya kwanza ya semi-pro ya usiku wa Solidarty & Fratenity Boxing Gala (Mshikamano na Udugu) tarehe 24 Januari, 2025 katika uwanja wa ndani wa Ammar Dakhlaoui, Tunis, Tunisia.

Katika pambano hilo la uzani wa Light Welterweight 63.5kg, Lucas aliibuka kwa ushindi wa majaji wote watatu (3).

Baada ya ushindi, Kocha wa timu ya taifa ya ngumi, Samweli Kapungu 'Batman' amesema siri ya ushindi wa bondia wake ni nidhamu ambayo imesababisha kupata matokeo mazuri.

Kapungu alisema amefurahishwa na matokeo hayo ambayo bondia wake amezingatia maelekezo aliyompatia.

Kwa upande wake bondia Mwajobaga alisema mkanda huo ni zawadi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Tumefungua mwaka vizuri kwa kuliheshimisha taifa letu Kimataifa, na ushindi huu wa mkanda wangu ni zawadi kwa Rais Dkt. Samia kutoka kwangu, "alisema Mwajobaga.