KLABU BINGWA NETIBOLI YAANZA KWA KISHINDO DAR

20 Jun, 2023
Mashindano ya klabu Bingwa taifa Netiboli yameanza kwa kishindo kwa michezo mitano kupigwa leo kwenye Uwanja wa nje wa Benjamini mkapa jijini Dar es Salaam.
Matokeo ya leo juni 20,2023 Tanroad imeanza kwa kuibuka na ushindi wa magoli 46-16 dhidi ya Upendo Queens, huku NSSF imekubali kichapo cha magoli 48 - 44 dhidi ya Jeshi star,wakati Nyika Queens imepoteza kwa magoli 79 - 18 dhidi ya JKT Mbweni.
Matokeo mengine Kampala imetoka kifua mbele dhidi ya Tanroad kwa kuifunga magoli 59-31, huku Maafande wa Jeshi Star wametoka na ushindi wa magoli 66 - 17 dhidi ya Upendo Queens.
Mashindano hayo yataendelea kesho kwa michezo 12 kuchezwa .