KUKABIDHIWA KWA BIMA ZA AFYA KWA MAVETERANI WA SOKA NCHINI.
service image
25 Apr, 2024


Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya michezo wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa, Bw. Ally Mayay amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kukaa kikao na vyama vya michezo na mashirikisho ya michezo kwa lengo la kujadili na kuangalia bajeti ya uwajibikaji kwa jamii “CSR “ ili kuwakatia bima za afya wachezaji wa zamani wa timu za taifa.

Mayay ameyasema hayo leo Aprili 25, 2024 wakati wa kukabidhi kadi za Bima ya afya kwa baadhi ya wachezaji wa soka wa zamani (UMSOTA) zilizodhaminiwa na Kampuni inayohusika na ngumi za kulipwa ya 'Toshi cargo' ambayo imedhamini kadi tano (5) za bima ya afya ya Taifa (NHIF) ambapo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) litagharamia kadi tano (5) za wanasoka hao wa zamani.