Ladies First 2023
service image
22 Nov, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha, Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ushirikiano wa Kimataifa la Japan (JICA) Ara Hitoshi, Mwenyekiti wa kamati ya Ufundi Shirikisho la Riadha Tanzania (AT) Michael Washa, Mwasisi wa 'Ladies First' Kanali Mstaafu Juma Ikangaa, wameshikana mikono kuonesha ushirikiano baina yao katika kuinua wasichana kupitia mchezo wa riadha. Tukio hilo wamelifanya leo Novemba 22, 2023 baada ya mkutano na waandishi wa habari wenye lengo kuutaarifu umma kuhusu mashindino ya riadha ya wanawake msimu wa tano (5) yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 24, 25 na 26 Novemba, 2023 jijini Dar es salaam.