LADIES FIRST 2023
service image
25 Nov, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha alisema lengo la mashindano ya riadha ya wanawake 'Ladies First' ni kuhamasisha na kuimarisha ushiriki wa wanawake katika michezo.

“Kwa miaka ya hivi karibuni tumeona jinsi wanawake wanavyofanya vizuri katika michezo, sababu kubwa ni pamoja na mashindano haya yenye lengo la kuendelea kuinua na kukuza michezo hasa katika mchezo wa riadha kwa wanawake,” alisema Msitha.

Naye Mwakilishi wa JICA Tanzania ambao ndio wadhamini wa mashindano hayo, Ara Hitoshi alisema Tamasha hilo ambalo mwasisi ni balozi wa hiari wa JICA Juma Ikangaa yanatoa fursa hasa kwa wanawake katika uelewa wa kijinsi na kujitambua.

“Jukumu la kuendeleza Michezo sio la Serikali bali ni la kila mtu kushiriki ili kuendeleza vipaji hasa kwa wanawake kuendelea kuongeza uelewa wa kijinsia kwa wanariadha wanawake,” alisema Ara.