LADIES FIRST 2023
service image
28 Nov, 2023

BMT yapewa hongera na JICA

Viongozi wa Shiriki la Maendeleo la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA) leo Novemba 28, 2023 wamefika katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuwashukuru kwa kukamilisha kwa mafanikio makubwa mashindano ya riadha ya wanawake yaliyopewa jina la 'Ikangaa Ladies First' msimu wa tano yaliyomalizika Novemba 26, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Jijini Dar es salaam.

Katika kikao chao kifupi cha tathmini pande zote pili, BMT na JICA wameonesha kufanikiwa kwa kiasi cha juu tofauti na miaka minne iliyotangulia, ikidhihirishwa na ushiriki mkubwa wa Mikoa karibu yote isipokuwa Mikoa miwili tu, ikiwemo Njombe na Latavi.

Aidha, Viongozi hao wamekubalina kujipanga vyema ikiwemo kufuata maelekezo ya Viongozi wa juu ili mashindano ya 2024 yawe na ubora zaidì