VIONGOZI WA VYAMA VYA MICHEZO WAASWA KUWA WABUNIFU KUENDELEZA MICHEZO NCHINI
service image
23 Nov, 2023

Viongozi wa Vyama vya Michezo nchini wametakiwa kuwa wabunifu, kujipambanua na kufanya ushawishi kwa wadau wa michezo Ili kuendeleza shughuli za michezo nchini.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha, baada ya kukabidhiwa baiskeli mwendo kwa ajili ya Chama cha Mchezo wa Kikapu cha Watu wenye za ulemavu Tanzania ( TWBA) vilivyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya msalaba mwekundu (ICRC), tukio lililofanyika kwenye ofisi za BMT jijini Dar es Salaam.



Kwa Upande wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Kikapu Kwa watu wenye Ulemavu Tanzania (TWBA) Abdallah Mpogole, alisema wamepokea baiskeli za michezo 12 Kwa ajili ya harakati za kuendeleza mchezo huo hapa nchini.

"Tunaishukuru ICRC kwa msaada huu ambao sio mara ya kwanza, mara nyingine tuliweza kupeleka, Mikoa ya Kilimanjaro, Iringa na Zanzibar, na nia yetu ni kufika Mikoa yote Ili mchezo huu, uchezwe kila Kona ya nchi,' alisema Mpogole.

Aidha, ameiomba BMT kuendelea kuwashika mkono pale watakapohitaji msaada wa kuwawezesha kuifikia jamii ya watu wenye Ulemavu waishio pembezoni ili nao washiriki katika michezo.