MICHEZO IENDELEE 0KUWA AJIRA NA UCHUMI
service image
10 Nov, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amezungumza na Msajili wa Vyama vya Michezo Wakili Evordy Kyando, Viongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) Viongozi PAF Promotion Kampuni iliyoanda pambano la Hassan Mwakinyo Septemba 29, 2023 pamoja na Viongozi wa Mwakinyo Promotion akiwemo Bondia Hassan Mwakinyo mara baada ya kikao kilichofanyika Novemba 7, 2023 Jijini Dar es Salaam

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vilivyokalia kati ya BMT, TPBRC, PAF na Mwakinyo Promotion kufuatia maelekezo ya Waziri kujadiliana na kufikia muafaka kufuatia sakata la Mwakinyo kutopanda ulingoni Septemba 29, 2023 na kupelekea kufungiwa na TPBRC mwaka mmoja na Faini ya Milioni 1.

Waziri amewataka wadau hao wa michezo kujadiliana na kupata suluhisho kwa manufaa ya pande zote na kwa maslahi ya Taifa.

"Wizara tumeondoka katika kuiona Utamaduni, Sanaa na Michezo ni burudani tu, sasa tuelemea katika sifa mbili Ajira na Uchumi," amesisitiza na kuongeza kuwa:

'Msajili utaniambia vyama vinavyofanya kazi ya kugombana badala ya kutengeneza ajira na uchumi tuvifute,"alisema.