MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA MICHEZO
service image
16 Oct, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo (BMT) Bi. Neema Msitha alimweleza Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dkt. Damas Ndumbaro kuwa, Baraza limeendelea kupata mafanikio mbalimbali kwa Timu za Taifa kupitia ufadhili wa Serikali chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Michezo kufika mashindano ya Fainali ya Kombe la Dunia kwa Timu ya Wanawake chini ya Miaka 17 pamoja na Timu ya Walemavu.

Msitha ameyasema hayo Oktoba 16 Oktoba, 2023 wakati wa kikao cha Waziri na Menejimenti ya Baraza hilo
Katika taarifa yake kwa Mhe. Waziri Msitha alimweleza kuwa, kwa sasa Baraza hilo linatumia mfumo wa Kidigitali kusajili Vyama na Mashirikisho ambao umerahisisha gharama na muda wa kufanya Usajili kwa sasa.