MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA MICHEZO.
service image
25 Apr, 2024

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha akielezea mafanikio ya sekta ya michezo leo Aprili 25, 2024 wakati wa matukio matatu muhimu sekta ya michezo, la kusainiwa kwa Mkataba wa ukarabati wa Uwanja wa Uhuru kati ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Kampuni ya ujenzi ya nchini China (CRCEG), uzinduzi wa Jarida la mafanikio katika sekta ya michezo ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, matukio hayo pia, yameambatana na kuzawadiwa kwa mabondia na viongozi wa Mchezo wa ngumi walioiwakilisha vyema nchi katika mashindano ya Afrika (All African Games) yaliyofanyika mwezi Machi 2024 nchini Ghana.