MAFUNZO YA USAJILI KWA MFUMO WA KIDIGITALI
service image
15 May, 2023

Kituo kwa Mei 15 ni Mkoa wa Iringa kuendelea na mafunzo ya mfumo wa usajili wa vyama vya michezo kidigitali yatayohusisha wasajili wasaidizi na viongozi wa vyama vya michezo kutoka katika halmashauri za Mkoa huo kuanzia tarehe 16 - 17 Mei, 2023 saa mbili (2:30) asubuhi katika Shule ya Sekondari ya Lugalo.

Waratibu wa mafunzo hayo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakiongozwa na Msajili wa vyama vya michezo nchini Rikizi Majala ambao wameripoti Ofisi ya Mkoa wa Iringa na kupokelewa na Katibu tawala msaidizi Deogratius Yinza, Afisa Elimu Mkoa Maria Lyimo pamoja na mwenyeji wao Afisa Utamaduni Steven Sanga ambao wameahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha mafunzo yanakuwa na tija kwa tasnia ya Michezo Mkoani hapo.