MAFUNZO YANAENDELEA
service image
16 May, 2023

Afisa Michezo kutoka BMT Abel Odena akitoa ufafanuzi wa nyaraka muhimu za kuambatanisha ili chama cha michezo kiweze kusajiliwa, ameyaeleza hayo wakati wa mafunzo ya usajili wa taasisi za michezo kidigitali yanayoendelea katika shule ya sekondari Lugalo Mkoani Iringa.

Nyaraka zinazotakiwa katika kusajili chama cha michezo ni pamoja na Muhtasari wa kikao cha wanachama kilichofikia uamuzi wa kuunda chama, nakala ya katiba, nakala ya kanuni za fedha, nakala ya kanuni za uendeshaji wa shughuli za chama, orodha ya wanachama, cheti cha usajili wa kampuni (Brela) pamoja na nakala laini ya sahihi ya mwenyekiti/rais na katibu wa chama.

Iringa ni Mkoa wa saba kunufaika na mafunzo hayo na Mkoa unafuata ni Morogoro kuanzia tarehe 18 hadi 19 Mei, 2023.