MAJALA AELEZA FAIDA ZA KUSAJILI TAASISI YA MICHEZO
service image
30 Sep, 2022

Msajili wa Vyama vya michezo nchini Riziki Majala amefafanua faida za Mtanzania yeyote anayetaka kufanya shughuli ya michezo kusajili taasisi yake.

Amefafanua kuwa usajili utamsaidia kutambulika rasmi na serikali pamoja na kuaminiwa na wafadhili, lakini pia kutanua wigo wa kueneza mchezo.

Aidha, Majala ameeleza baadhi ya changamoto Ofisi yake inazokutana nazo kuwa ni pamoja na wadau kunakili katiba zingine na kubadili jina pekee bila kujali lengo la yeye kuanzisha taasisi husika pamoja na kutojua umuhimu wa kuwa na kanuni za kuendesha taasisi husika