MALIASILI WAMPA UBALOZI WA UTALII WA HIARI RIO FERDINAND
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametangaza kumpa Ubalozi wa hiari wa Utalii wa Tanzania Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United na Timu ya Taifa ya Uingereza Rio Ferdinand.
Ubalozi huo umetangazwa tarehe 21 Mei, 2026 jijini Arusha, ambapo Mhe. Dkt. Ashatu ameeleza kuwa sekta ya utalii inaingiza kiasi cha sh Bil.4.4 kwa mwaka.
"Rio ana wafuasi katika mitandao ya kijamii, ambapo yeye kuitaja Tanzania kufuatia ziara aliyoifanya atawashawishi wafuasi hao kuja kutalii hapa Tanzania" amesisitiza Mhe. Ashatu.
Dkt. Ashatu ameongeza kuwa, hatua hiyo ni mojawawapo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo imeelekeza kufikia watalii milionii 8 kwa mwaka mmoja.
Aidha, amempongeza Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kumleta mchezaji huyo nchini, ambapo ni njia mojawapo ya kutangaza nchi na vivutio vyake kimataifa.
Kwa upande wake mchezaji Rio ameshukuru ukarimu na hesehima aliyoipata, akiahidi kuitangaza Tanzania na kurudi tena kutembea.

