MAPOKEZI YA TAIFA STARS.
08 Jan, 2026
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Miguel Gamondi, akipokea zawadi mbalimbali ikiwemo jogoo kutoka kwa mashabiki, ambapo jogoo mwingine pia alikabidhiwa kwa Nahodha wa Timu ya Taifa, Bakari Mwamnyeto, kama ishara ya pongezi kufuatia mafanikio ya kihistoria ya Taifa Stars kufuzu kwa mara ya kwanza hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), leo Januari 08, 2026 mara baada ya kuwasili nchini wakitokea Morocco.

