MASHINDANO YA KANDA YA TANO MPIRA WA KIKAPU

18 Jun, 2023
Timu ya taifa ya mpira kikapu wanaume (Tanzanite) imeanza vyema katika mashindano ya kanda ya tano yaliyofanyika jana juni 17 , 2023 kwenye uwanja wa ndani wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.
Tanzania iliiibuka na ushindi wa vikapu 69-34 dhidi ya Eritrea katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja ndani.
Mashindano hayo yameshirikisha nchi 10 na lengo ni kutafuta timu zitazofuzu kucheza mashindano ya Afrika.