Mhe. Paul Makonda (MB), ahudhulia mchezo wa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Timu ya Taifa ya Uganda
28 Dec, 2025
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (MB), alihudhuria mchezo wa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Timu ya Taifa ya Uganda katika mashindano ya AFCON uliofanyika mjini Rabat, nchini Morocco. Katika tukio hilo, Mhe. Makonda alikuwa pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, pamoja na viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika.
Ushiriki huo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha na kudumisha mahusiano mazuri na wadau wa soka barani Afrika na duniani kwa ujumla, sambamba na kukuza diplomasia ya michezo na maslahi ya maendeleo ya soka la Tanzania.

