MHE. RAIS AWAPATIA TAIFA STARS NDEGE YA KUWAFUATA NCHINI MOROCCO
07 Jan, 2026
Ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kuwabeba wachezaji na viongozi wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), imeondoka kuelekea Rabat, Morocco.
Safari hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kushiriki hatua ya 16 bora ya Fainali za TotalEnergies AFCON, hatua ambayo Taifa Stars imefuzu kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo, na hivyo kuiandikia Tanzania ukurasa mpya wa kihistoria katika soka la Afrika.
Mafanikio haya ni ushahidi wa kazi kubwa iliyofanywa na wachezaji, benchi la ufundi pamoja na mchango wa Serikali katika kuendeleza michezo nchini

