MHESHIMIWA PINDI CHANA ATOA WITO WANAWAKE KUSHIRIKI MICHEZO
service image
21 May, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa Wanawake kujitokeze kwa wingi kushiriki michezo mbalimbali ukiwemo wa Gofu kwa kuwa katika dunia ya sasa michezo inatoa fursa ya ajira.

Mhe. Waziri ametoa wito huo tarehe 21 Mei, 2023 wakati akifunga Mashindano ya Gofu ya Lugalo Ladies Open 2023 yaliyofanyika katika viwanja vya klabu ya mchezo Gofu iliyopo Lugalo Jijini Dar es salaam.

"Nalipongeza JWTZ na Klabu ya Gofu Lugalo kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi kutumia Klabu hii katika kuendeleza vipaji vyao na kukuza mchezo wa Gofu ambao unaendelea kukua siku hadi siku" amesema Mhe.Pindi.

Awali Mwenyekiti wa Lugalo Gofu Club Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo amesema mashindano hayo yameshirikisha wanamichezo takriban 100 ambapo Wanawake ni zaidi ya 50.