MICHEZO KUTUMIKA KUIMARISHA USHIRIKIANO
service image
21 May, 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dokta Pindi Chana amesema serikali itaendelea kutumia michezo kuumarisha umoja na ushirikiano kwa nchi za Afrika na duniani kiujumla.

Dokta Pindi Chana amesema hayo tarehe 21 Mei, 2023 wakati wa bonanza la michezo kuelekea kuadhimisha siku ya afrika Mei 25, 2023 tukio lililoandaliwa na Umoja wa wanadiplomasia wa Afrika lililofanyika katika kituo cha JK park Dar es salaam.

Katika hafla hiyo imechezwa michezo mitatu baina ya timu ya Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki dhidi ya timu ya Mabalozi wa nchi za Afrika nchini Tanzania
zikihusisha timu za wanaume, Wanawake na watoto.

Waziri Pindi katika tukio pia ametoa pongezi kwa timu za Simba na Yanga kwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.