MIKAKATI YA KUBORESHA MBIO YA KILI MARATHON.

09 Apr, 2024
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha, leo tarehe 9 Aprili, 2024 amekutana na wandaaji wa mbio ya Kili Marathon kujadili maendeleo ya mbio hiyo, maeneo gani yanayohitaji kuboreshwa, ikiwemo ushiriki wa wanariadha kutoka nje ya nchi kupata urahisi wa kushiriki pamoja na idadi yao.
Kikao hicho kimefanyika ofisini kwake Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.