KAMATI YA HAMASA TIMU ZA TAIFA YAKUTANA KUWEKA MIKAKATI
service image
06 Jan, 2024

Zaidi ya bilioni 10 zinatarajiwa kukusanya katika harambee ya kuchangia timu za taifa itakayofanyika Januari 10 Mwaka huu Kwenye hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa Habari Januari 06, 2024 katika Ukumbi ya Serena Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa, alisema kuwa fedha hizo ni Kwa ajili ya kuziwezesha timu za taifa zinapokwenda kushiriki mashindano mbalimbali ya Kimataifa na uchangiaji huo ni endelevu.

Alisema kuwa tayari Kamati ya hamasa imeundwa na kugawanywa katika makundi mawili ambapo ipo Kamati ndogo ya Fedha na Mipango pamoja na kamati ndogo ya hamasa.

"Tuna Kamati mbili ambayo niya fedha na mipango itakayokuwa na jukumu la kutengeneza mipango ya kutafuta fedha zitakazosaidia kugharamia timu za taifa na kamati ya hamasa itahamasisha wadau kuunga mkono nguvu ya Rais Samia kuchangia timu za taifa pamoja na kuhamasisha washabiki wajae uwanjani kwa wingi kuzishangilia timu uwanjani,"alisema na kuongeza kuwa;

"Tunataka kufika mbali zaidi ya Afcon katika soka na mashindano ya michezo mingine,".