MSIGWA: VYAMA VYA MICHEZO VIACHE MIGOGORO

Katibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amevitaka vya vya michezo kuongea lugha moja kwa ajili ya maslahi ya Taifa.
Amesema vyama hivyo kuachana na migogoro na kutumia mitandao ya kijamii kwa kusema mambo mazuri kwa ajili ya kujiweka sifa ya nchini.
“Hivi kwa sasa tuna uwenyeji wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN 2024 na AFCON 2027. Viongozi wa vyama vya michezo kuepusha migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na kuepuka na taarifa mbaya za Taifa katika mitandao ya kujamii.
"Tukitumia mitandano kwa kuweka migogoro na sambaza katika mitandao mambo ambayo yanayochechea uvunjaji wa amani basi hili suala la kupewa uwenyeji wa mashindano yatafutwa,” amesema.
Msigwa amesema tunapoenda kwenye uwekezaji mkubwa nchi inapaswa kuongee lugha moja kwa kuwa hakuna mwekezaji anayekuja kuweka fedha katika sehemu yenye migogoro.