MWAKINYO AOMBA RADHI KUSAFIRI BILA KIBALI CHA BMT

Bondia Hassan Mwakinyo ameiomba radhi Serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa (TPBRC) kwa kusafiri bila kibali cha Baraza kuelekea nchini Uingereza kushiriki pambano dhidi ya bondia Liam Smith lililofanyika tarehe 03 nchini humo.
Radhi hiyo ameiomba leo Septemba 30, 2022 katika kikao alichoitwa na Baraza ili kutoa sababu za yeye kusafiri bila kuwa na kibali, ambapo alieleza kuwa kuchelewa kwa viza ndiko kuliko sababisha yeye kuondoka bila kuwa na kibali.
Mwenyekiti wa kikao hicho na Afisa Michezo Mkuu Allen Allex kwa niaba ya Katibu Mtendaji amewataka TPBRC kusimamia taratibu zote zinazotakiwa kwa bondia kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya pambano.
"Taratibu za kuomba visa lazima ziende sambamba na kuomba kibali cha kisafiri,"alisema Allen.
Kwa upande wake Katibu wa TPBRC Yahya Poli amesema kuwa, watatoa taarifa rasmi kwa wadau kuhusu tukio hilo.