NAIBU KATIBU MKUU SERERA APOKELEWA BAADA YA UAPISHO.
service image
04 Apr, 2024

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dokta Suleiman Hassan Serera amewataka wafanyakazi wa wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuendelea kuenzi matarajio ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan, Ilani pamoja na wizara kwa ujumla.

Dkt. Serera ameyasema hayo leo tarehe 4 Aprili, 2024 alipokutana na wafanyakazi wa wizara waliopo uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo ameahidi kutoa ushirikiano wa katosha kwa wafanyakazi wote ili kuendeleza gurudumu la Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini.