NAIBU WAZIRI MAKONDA AWAPA MORALI TAIFA STARS
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Christian Makonda, ametoa hamasa na morali kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) pamoja na benchi la ufundi, alipokutana nao katika hoteli ya Barcelo Convention Center, jijini Fes, Morocco, ambako timu hiyo imeweka kambi ya maandalizi.
Akizungumza na wachezaji na benchi la ufundi, Mhe. Makonda aliwasisitiza wachezaji kupambana kwa moyo wote, nidhamu na uzalendo wanapoivaa jezi ya Taifa, akibainisha kuwa Watanzania wote wako nyuma yao kwa kuwaunga mkono, kuwashangilia na kuwaombea ili waweze kuliletea Taifa heshima.
“Taifa zima lina imani kubwa nanyi. Chezeni kwa moyo, kwa umoja na kwa kujituma, mkijua mna mamilioni ya Watanzania wanaowaombea na kuwaunga mkono,” alisema Mhe. Makonda.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza tarehe 23 Desemba, 2025, katika mji wa Fes, Morocco, dhidi ya Timu ya Taifa ya Nigeria.

