NMB YATOA ZAWADI KWA BMT
29 Dec, 2025
Kaimu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Thadeus Almas,leo tarehe 29 Desemba, 2025 amepokea zawadi kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Kurasini,Bi. Veronica Mbawa, kama ishara ya kuthamini ushirikiano wao wa kibiashara.
Zawadi hiyo imetolewa na Benki ya NMB kwa BMT ikiwa ni mteja wao, hatua inayodhihirisha mahusiano mazuri na endelevu kati ya Taasisi hizo mbili.

